JINA LA NCHI
Bio‑Oil®
JINA LA BIDHAA NA UKUBWA
Skincare Oil 25ml
Skincare Oil 60ml
Skincare Oil 125ml
Skincare Oil 200ml
DALILI
Makovu Husaidia kuboresha mwonekano wa makovu mapya na ya zamani. Michirizi kwenye ngozi Husaidia kuboresha mwonekano wa michirizi kwenye ngozi. Pia husaidia kuboresha mnyumbuko wa ngozi, na hivyo kupunguza uwezekano wa michirizi kwenye ngozi kutokea. Rangi ya ngozi isiyo sawia Husaidia kuboresha mwonekano rangi ya ngozi isiyo sawia. Kuzeeka kwa ngozi Husaidia kuboresha mwonekano wa kuzeeka kwa ngozi kwenye uso na mwili. Ngozi iliyokauka Husaidia kupunguza upotezaji wa unyevu na huboresha mwonekano wa ngozi iliyokauka.
ONYESHO
Mafuta ya rangi ya machungwa / waridi.
MUUNDO
Mchanganyiko wa mafuta maalum na vitamini na vitu vilivyotolewa katika mimea.
VIUNGO
Paraffinum Liquidum, Triisononanoin, Cetearyl Ethylhexanoate, Isopropyl Myristate, Retinyl Palmitate, Helianthus Annuus Seed Oil, Tocopheryl Acetate, Anthemis Nobilis Flower Oil, Lavandula Angustifolia Oil, Rosmarinus Officinalis Leaf Oil, Calendula Officinalis Extract, Glycine Soja Oil, Bisabolol, Tocopherol, Parfum, Alpha-Isomethyl Ionone, Amyl Cinnamal, Benzyl Salicylate, Citronellol, Coumarin, Eugenol, Farnesol, Geraniol, Hydroxycitronellal, Limonene, Linalool, CI 26100.
VITU VISABABISHAVYO MIZIO
Kuna vitu 11 visababishavyo mizio katika Bio‑Oil® Skincare Oil. Kama ilivyo na vitu vingi visababishavyo mizio, hivi vipo katika mafuta ya mimea na manukato. Hivyo ni: Alpha-Isomethyl Ionone, Amyl Cinnamal, Benzyl Salicylate, Citronellol, Coumarin, Eugenol, Farnesol, Geraniol, Hydroxycitronellal, Limonene, na Linalool.
TATHMINI YA USALAMA
Bio‑Oil® Skincare Oil imefanyiwa tathmini ya usalama na mtaalamu wa sumu aliyehitimu na imeainishwa kuwa salama kwa matumizi yake yaliyokusudiwa na watu wazima, ikiwa ni pamoja na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, na watoto zaidi ya umri wa miaka mitatu.
JARIBIO LA KIMATIBABU LA MAKOVU
Kituo cha majaribio proDERM Institute for Applied Dermatological Research, Hamburg, Germany. Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa makovu. Sampuli Wahusika: Washiriki 36 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick. Umri wa makovu: yaliyotokea hivi karibuni hadi miaka 3. Maeneo ya makovu: fumbatio, mguu, mkono, shingo, goti, kiwiliwili, mwili wa juu. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti fiche, wa nasibu na unaothibitiwa wa kipozauongo. Wahusika walikuwa na makovu yanayolingana au kovu linalotosha kuruhusu matumizi nusu nusu ya kovu na uwezo wa kulinganisha wahusika. Bidhaa ilitumiwa mara mbili kila siku kwa wiki 8; hakuna usingaji wa ziada uliyofanywa kwenye eneo lengwa. matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika vipindi vya mara kwa mara. Tathmini zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4 na 8. Vigezo tofauti vya kovu kama ilivyofafanuliwa katika Mizani ya Tathmini ya Makovu kutoka kwa mtazamo wa Mgonjwa na Daktari (POSAS) vilitathminiwa. Matokeo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa makovu. Matokeo muhimu kitakwimu yalipatikana baada ya wiki 2 tu (siku ya 15), yaliyoshuhudiwa katika asilimia 66% ya wahusika. Baada ya wiki 8 (siku ya 57) asilimia 92% ya wahusika walionekana kupata nafuu, huku kiwango cha kupata nafuu kikiwa karibu mara tatu ya wiki ya 2. Unafuu endelevu wa POSAS katika muda wa utafiti huu.
UTAFITI WA MAKOVU YA CHUNUSI
Kituo cha majaribio
Dept. of Dermatology, Peking University First Hospital, Beijing, China.
Lengo
Utafiti wa kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa makovu ya chunusi kwenye uso wa wahusika Wachina.
Sampuli
Wahusika:
Wahusika 44 wa Kichina wenye makovu mapya ya chunusi usoni (
JARIBIO LA KIMATIBABU LA MICHIRIZI KWENYE NGOZI
Kituo cha majaribio proDERM Institute for Applied Dermatological Research, Hamburg, Germany. Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa michirizi kwenye ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 38 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick. Sababu za michirizi kwenye ngozi. mbalimbali (baada ya ujauzito, kuongezeka kwa uzani au ukuaji wa haraka katika miaka ya ujana). Maeneo ya michirizi kwenye ngozi: tumbo, mapaja na nyonga. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti fiche, wa nasibu na unaothibitiwa wa kipozauongo. Wahusika walikuwa na michirizi inayolingana kwenye ngozi au michirizi kwenye ngozi inayotosha kuruhusu matumizi nusu nusu kwenye michirizi na uwezo wa kulinganisha wahusika. Bidhaa ilitumiwa mara mbili kila siku kwa wiki 8, hakuna usingaji wa ziada uliyofanywa kwenye eneo lengwa. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika vipindi vya mara kwa mara. Tathmini zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4 na 8. Vigezo tofauti vya kovu kama ilivyofafanuliwa katika Mizani ya Tathmini ya Makovu kutoka kwa mtazamo wa Mgonjwa na Daktari (POSAS) vilitathminiwa. Matokeo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa michirizi kwenye ngozi. Matokeo muhimu kitakwimu yalipatikana baada ya wiki 2 tu (siku ya 15), yaliyoshuhudiwa katika asilimia 95% ya wahusika. Baada ya wiki 8 (siku ya 57) asilimia 100% ya wahusika walionekana kupata nafuu, huku kiwango cha kupata nafuu kikiwa karibu mara mbili ya wiki ya 2. Unafuu endelevu wa POSAS katika muda wa utafiti huu.
JARIBIO LA KIMATIBABU LA RANGI YA NGOZI ISIYO SAWIA
Kituo cha majaribio Thomas J. Stephens & Associates, Inc., Texas, United States of America. Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa rangi ya ngozi isiyo sawia na rangi isiyolingana wakati inatumiwa na wanawake wenye ngozi inayoathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua (kuzeeka) kwenye uso na shingo. Sampuli Wahusika: Washiriki 67 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick waliobainishwa kimatibabu kuathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua kwenye uso na shingo. Washiriki waliotibiwa kwa Bio‑Oil Skincare Oil® walikuwa wahusika 35 na washiriki wasiotibiwa walikuwa wahusika 32. Umri wa washiriki: 30–70. Mbinu Utafiti unaomficha mhusika, unaodhibitiwa na wa nasibu. Wahusika walishiriki katika tathmini ya kwanza ya uchunguzi ikifuatiwa na kipindi cha kuondoa matibabu cha wiki 1. Bidhaa ilitumiwa kwenye uso na shingo mara mbili kila siku kwa wiki 12. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika ziara rasmi ya kwanza. Tathmini za kimatibabu zilizofanywa katika wiki ya 0, 2, 4, 8 na 12. Wahusika walipewa alama tofauti za kimatibabu kwenye uso na shingo ili kuangalia rangi ya ngozi isiyo sawia na rangi isiyolingana. Matokeo Ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa rangi ya ngozi isiyo sawia na rangi isiyolingana katika ngozi inayoathiriwa na mwangaza jua (kuzeeka). Baada ya wiki 4 matokeo muhimu kitakwimu yalipatikana katika vigezo vyote kwenye uso na shingo. Baada ya wiki 12, asilimia 86% ya wahusika wanaotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil walionyesha kuimarika pakubwa kitakwimu katika rangi ya ngozi isiyo sawia kwenye uso, asilimia 71% ya wahusika katika rangi isiyolingana kwenye uso, asilimia 69% katika rangi ya ngozi isiyo sawia kwenye shingo na asilimia 60% katika rangi isiyolingana kwenye shingo.
JARIBIO LA KIMATIBABU LA KUZEEKA KWA NGOZI
Kituo cha majaribio Thomas J. Stephens & Associates, Inc., Texas, United States of America. Utafiti wa 1: Uso na shingo Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil ikitumiwa na wanawake wenye ngozi inayoathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua (kuzeeka) kwenye uso na shingo. Sampuli Wahusika: Washiriki 67 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick waliobainishwa kimatibabu kuathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua kwenye uso na shingo. Washiriki waliotibiwa kwa Bio‑Oil Skincare Oil® walikuwa wahusika 35 na washiriki wasiotibiwa walikuwa wahusika 32. Umri wa washiriki: 30–70. Mbinu Utafiti unaomficha mhusika, unaodhibitiwa na wa nasibu. Wahusika walishiriki katika tathmini ya kwanza ya uchunguzi ikifuatiwa na kipindi cha kuondoa matibabu cha wiki 1. Bidhaa ilitumiwa kwenye uso na shingo mara mbili kila siku kwa wiki 12. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika ziara rasmi ya kwanza. Tathmini za kimatibabu zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4, 8 na 12. Wahusika walipewa alama tofauti za kimatibabu kwenye uso na shingo kwa vigezo vifuatavyo vya ufanisi: mwonekano wa jumla, mistari laini, makunyanzi makubwa, rangi isiyolingana, rangi ya ngozi isiyo sawia, mwonekano wa kuparara / ulaini, hisia ya kuparara / ulaini, mwonekano thabiti, na wangavu (kutong’aa). Matokeo Ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa jumla katika ngozi inayoathiriwa na mwangaza jua (kuzeeka) kwenye uso na shingo. Baada ya wiki 8 matokeo muhimu kitakwimu yalipatikana katika vigezo vyote vya vya ufanisi vilivyopewa alama za kimatibabu. Baada ya wiki 12 asilimia 94% ya wahusika waliotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil walionyesha kuimarika pakubwa kitakwimu katika mwonekano wa jumla kwenye uso na asilimia 80% ya wahusika walionyesha kuimarika pakubwa kitakwimu katika mwonekano wa jumla kwenye shingo. Utafiti wa 2: Mwili Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil ikitumiwa kwenye ngozi ya sehemu ya juu ya kichwa, mguu wa chini na mkono na wanawake wenye ngozi inayoathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua (kuzeeka). Sampuli Wahusika: Washiriki 67 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick waliobainishwa kimatibabu kuathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua kwenye uso na shingo. Washiriki waliotibiwa kwa Bio‑Oil Skincare Oil® walikuwa wahusika 35 na washiriki wasiotibiwa walikuwa wahusika 32. Umri wa washiriki: 30–70. Mbinu Utafiti unaomficha mhusika, unaodhibitiwa na wa nasibu. Wahusika walishiriki katika tathmini ya kwanza ya uchunguzi ikifuatiwa na kipindi cha kuondoa matibabu cha wiki 1. Bidhaa ilitumiwa kwenye kwa sehemu ya juu ya kichwa, miguu ya chini na mikono mara mbili kila siku kwa wiki 12. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika ziara rasmi ya kwanza. Tathmini za kimatibabu zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4, 8 na 12. Wahusika walipewa alama tofauti za kimatibabu za sehemu ya juu ya kichwa, miguu ya chini na mikono kulingana na vigezo vifuatavyo vya ufanisi: mwonekano wa jumla, makunyanzi makubwa, ukavu / magamba, mwonekano wa kuparara / ulaini, na hisia ya kuparara / ulaini. Matokeo Ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil katika kuboresha mwonekano wa jumla katika ngozi inayoathiriwa na mwangaza jua (kuzeeka) kwenye mwili. Baada ya wiki 4 matokeo muhimu kitakwimu yalipatikana katika vigezo vyote vya vya ufanisi vilivyopewa alama za kimatibabu. Baada ya wiki 12 asilimia 89% ya wahusika waliotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil walionyesha kuimarika pakubwa kitakwimu katika mwonekano wa jumla wa sehemu ya juu ya kichwa, miguu ya chini na mikono.
JARIBIO LA KIMATIBABU LA KUZEEKA KWA NGOZI
Kituo cha majaribio Photobiology Laboratory of the Medical University of South Africa. Utafiti wa 1: Unyevu wa ngozi ya juu zaidi na kazi ya kuzuia Lengo Kutathmini athari za kutumia mara moja Bio‑Oil® Skincare Oil ili kuboresha kazi ya ngozi ya juu zaidi (SC) na unyevu. Sampuli Wahusika: Washiriki 40 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick. Eneo la jaribio: bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa kwenye mkono wa mbele wa wahusika wote. Mbinu Tathmini ya unyevu wa ngozi kwa kutumia Corneometer kama kipimo msingi, tathmini ya kazi ya kuzuia kwa kutumia Vapometer kama kipimo cha pili. Washiriki waliosha vigasha vyao kwa sabuni saa 2 kabla ya vipimo kuchukuliwa ili kusababisha ukavu wa ngozi. Vipimo msingi vya kifani vilichukuliwa. Bio‑Oil® Skincare Oil na mafuta ya ukadiriaji yalitumiwa kwenye maeneo tofauti ya mkono wa mbele wa wahusika wote. Vipimo vilichukuliwa tena mara moja baada ya matumizi ya bidhaa na saa 2 baadaye, kabla na baada ya kuondoa bidhaa. Eneo lisilotibiwa lilipimwa pia nyakati zote. Matokeo Baada ya matumizi ya papo hapo, mafuta yote yalipunguza maji yanayotoka kwenye ngozi (TEWL) ikilinganishwa na wale wasiotibiwa. Thamani iliyoongezeka ya uwezo wa ngozi katika muda wa saa 2 kabla ya kuondoa bidhaa ilionyesha kuongezeka kwa unyevu wa ngozi kwa mafuta yote mawili. Saa mbili baadaye, baada ya kuondoa mafuta kwenye uso, Bio‑Oil® Skincare Oil ilionyesha ongezeko zaidi la thamani za TEWL ikilinganishwa na mafuta ya ukadiriaji, hivyo kuonyesha kuongezeka kwa unyevu na kwa hivyo kuongezeka kwa uyenvu wa ngozi. Utafiti wa 2: Mwonekano wa ngozi kavu Lengo Kutathmini athari za matumizi ya mara mbili ya kila siku ya Bio‑Oil® Skincare Oil kwa ajili ya utendaji wa ulainishaji na utulizaji wa ngozi kavu. Sampuli Wahusika: Washiriki 25 wa kike Wazungu. Eneo la jaribio: bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa kwenye sehemu ya nje ya mguu wa chini wa wahusika wote. Mbinu Sabuni ilitumiwa ili kufanya ngozi kuwa kavu kwa kipindi cha siku 7. Bio‑Oil® Skincare Oil na mafuta ya ukadiriaji yalitumiwa mara mbili kila siku. Uchunguzi wa ngozi ulifanywa siku ya 1 na 3. Tathmini za kuangalia zilifanywa na mtathmini mtaalamu wa kuangalia kwa kutumia taa ya kukuza 2x. Eneo lisilotibiwa lilitathminiwa pia nyakati zote. Matokeo Bio‑Oil® Skincare Oil na mafuta ya ukadiriaji yaliboresha ukavu wa ngozi ikilinganishwa na wahusika wasiotibiwa. Bio‑Oil® Skincare Oil ilikuwa bora zaidi kitakwimu katika siku ya 3. Maboresho makubwa katika mwonekano wa kuona wa maeneo ya ngozi yaliyotibiwa na kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil yalithibitisha ufanisi wake katika kupunguza ngozi kavu.
JARIBIO KWENYE NGOZI INAYOATHIRIKA KWA URAHISI
Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Kutathmini uwezo wa Bio‑Oil® Skincare Oil kusababisha mwasho wa ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 25; 19 wa kiume na 6 wa kike, wote wakiwa na ngozi inayoathirika kwa urahisi kulingana na jaribio la kuathiriwa na asidi ya maziwa. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti wa nasibu na unaodhibitiwa. Maeneo mawili yalitathminiwa: eneo ambalo udhibiti hasi ulitumika (maji yaliyosafishwa) na eneo ambalo Bio‑Oil® Skincare Oil ilitumika. Bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa nyuma ya mikono ya washiriki kwa kipindi cha saa 48 kwa kutumia Finn Chamber®. Matokeo ya ngozi yalitathminiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi, ili kutathmini mwasho wa kwanza wa ngozi kwa dakika 15, saa 1 na saa 24 baada ya kuondolewa kwa pamba. Matokeo ya ngozi yalikadiriwa kwenye mizani inayoanzia 0-4 (huku 0 ikiwa hakuna harara, uvimbe, au aina nyingine za mwasho wa ngozi, na 4 ikiwa harara na uvimbe mkali, inayoashiria mwonekano wa rangi nyekundu iliyokolea na uvimbe ulioenea zaidi ya eneo lililotumika). Matokeo Hakuna wahusika waliopata madhara yoyote mabaya yanayotokana na bidhaa inayojaribiwa, ikiwa na alama ya kuangalia ya 0 (sufuri) iliyorekodiwa kwa wahusika wote nyakati zote. Uwezo wa ngozi kustahimili Bio‑Oil® Skincare Oil ulichukuliwa kuwa ''usiowasha''.
JARIBIO LA KUTOSABABISHA CHUNUSI
Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Ili kujaribu ikiwa Bio‑Oil® Skincare Oil inaweza kusababisha chunusi na mabaka (chunusi). Sampuli Wahusika: Washiriki 20; 14 wa kike na 6 wa kiume wenye aina tofauti za ngozi ya Fitzpatrick na wanaoweza kuathiriwa na chunusi. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti wa nasibu na unaodhibitiwa. Bidhaa hiyo ilitumiwa kwenye karatasi ya ufyonzaji na kupakwa kwenye eneo la juu la migongo ya washiriki. Pamba hizo ziliachwa kwa saa 48 hadi 72, zikaondolewa na kutumiwa tena. Jumla ya pamba 12 zilitumika kwa wiki 4 mfululizo. Maeneo matatu yalitathminiwa kwa kulinganisha udhibiti hasi (maji yaliyosafishwa), bidhaa inayojaribiwa (Bio‑Oil® Skincare Oil) na udhibiti chanya (kileo cha lanolini, bidhaa inayojulikana kusababisha chunusi). Matokeo ya ngozi yatathminiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi dakika 15 baada ya kuondolewa kwa kila pamba ili kulinganisha uwepo wa mabaka kabla na baada ya kutumiwa kwa kila bidhaa. Matokeo Bio‑Oil® Skincare Oil ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Eneo ambalo Bio‑Oil® Skincare Oil ilitumika halikuonyesha tofauti kubwa ikilinganishwa na eneo la udhibiti hasi. Udhibiti chanya ulisababisha chunusi.
UTAFITI WA UFYONZAJI
Kituo cha majaribio proDERM Institute for Applied Dermatological Research, Hamburg, Germany. Utafiti wa 1: Wakadiriaji wataalamu Lengo Kutathmini kiwango cha ufyonzaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil baada ya matumizi ya kawaida na kusugua. Sampuli Wahusika: Wakadiriaji 22 wataalamu; 21 wa kike na 1 wa kiume. Eneo la jaribio: bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa kwenye mkono wa mbele wa wakadiriaji wote. Mbinu Utafiti fiche, wa nasibu na unaothibitiwa. Bio‑Oil® Skincare Oil na mafuta ya ukadiriaji yalitumiwa kwenye maeneo yaliyoteuliwa ya mkono wa mbele wa wakadiriaji wote. Wakadiriaji walitekeleza mienendo 100 ya kuendesha baisikeli kwa kasi iliyobainishwa. Kisha wakadiriaji walikadiria ufyonzaji wa bidhaa kwenye mizani ya alama 5 kuanzia ''inafyonza polepole sana'' hadi ''inafyonza haraka sana''. Vipimo vya Sebumeter, vya kutathmini kiasi cha mafuta kwenye ngozi, vilichukuliwa mara mbili kwa wakati tofauti; Kabla ya kutumia na dakika 2 baada ya kutumia bidhaa. Matokeo Ufyonzaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil kwenye ngozi ulitathminiwa kuwa ''wa haraka sana'' au ''wa haraka'' na wengi (asilimia 77.3%) ya wakadiriaji wataalamu. Hii ilithibitishwa kupitia kipimo kifani kwa kutumia usomaji wa sebumeter wakati wa pili ambao ulionyesha kuwa kiasi cha Bio‑Oil® Skincare Oil kilichobaki kwenye ngozi kilikuwa chini sana ikilinganishwa na mafuta ya ukadiriaji. Utafiti wa 2: Jopo la watumiaji Lengo Kutathmini kiwango cha ufyonzaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil baada ya matumizi ya kawaida na kusugua. Sampuli Wahusika: Washiriki 100; 97 wa kike na 3 wa kiume. Eneo la jaribio: bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa kwenye mkono wa mbele wa washiriki wote. Mbinu Utafiti fiche, wa nasibu na unaothibitiwa. Bio‑Oil® Skincare Oil na mafuta ya ukadiriaji yalitumiwa kwenye maeneo yaliyoteuliwa ya mkono wa mbele wa washiriki wote. Washiriki walisugua bidhaa inayojaribiwa kwa dakika moja kila mmoja. Kisha washiriki walikadiria ufyonzaji wa bidhaa kwenye mizani ya alama 5 kuanzia ''inafyonza polepole sana'' hadi ''inafyonza haraka sana''. Matokeo Ufyonzaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil kwenye ngozi ulitathminiwa kuwa ''wa haraka sana'' au ''wa haraka'' na wengi (asilimia 72%) ya washiriki.
UTAFITI WA UWEZO WA KUZIBA
Kituo cha majaribio Jaribio lilifanywa na Dkt. J Wiechers katika Maabara ya Rigano, Milan, Italia. Lengo Kutathmini kama Bio‑Oil® Skincare Oil inaonyesha kiwango sawa cha kuziba kama utando unaolinda ngozi ya kijusi. Utando unaolinda ngozi ya kijusi unazingatiwa sana na wanasayansi wa vipodozi kama ''kipimo bora zaidi'' katika ulainishaji wa ngozi kwa sababu ya kiwango chake bora cha kuziba. Mbinu Kiasi kinachojulikana cha maji kiliwekwa katika bika kikiwa kimefunikwa kwa utando unaoweza kupenyeza nusu uitwao Vitro-Skin™, ambao unaiga sifa za sehemu ya juu ya ngozi ya binadamu. Kiasi sawa cha utando unaolinda ngozi ya kijusi na Bio‑Oil® Skincare Oil kilitumiwa kwenye utando na kiwango cha kupoteza maji kutoka kwenye bika kilipimwa over time. Hii ililinganishwa na kiwango cha kupoteza maji bila bidhaa yoyote kwenye utando. Kiwango cha uhamishaji wa mvuke wa maji kwa kila bidhaa kilihesabiwa na kuonyeshwa katika g / m2 / h. Matokeo Bio‑Oil® Skincare Oil ilionyesha kiwango sawa cha kuzia kama utando unaolinda ngozi ya kijusi, iliandikisha 23.5 ikilinganishwa na 27.2 ya utando unaolinda ngozi ya kijusi.
MATUMIZI
Jinsi ya kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil inapaswa kusingwa kwa mwendo wa mviringo kwenye mwili hadi ifyonzwe kabisa. Inashauriwa kwamba bidhaa hiyo itumiwe mara mbili kwa siku, kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu. Bio‑Oil® Skincare Oil haipaswi kutumiwa kwenye kidonda wazi au ngozi iliyokatika. Imekusudiwa kutumiwa kama kipodozi tu. Ni salama kutumia kwenye kovu mara tu ngozi iliyo juu imepona kabisa. Matokeo yatatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Muda wa kutumia Jaribio la kimatibabu la Bio‑Oil® Skincare Oil limefanywa kwa kipindi cha wiki 8 na wiki 12, hivyo kuruhusu utendaji wa bidhaa hiyo kutathminiwa baada ya muda. Uchambuzi wa takwimu unaonyesha uboreshaji mkubwa katika mwonekano wa ngozi baada ya muda mfupi kama wiki mbili na kwamba uboreshaji huu unadumishwa au huongezeka kwa muda wa majaribio yote. Tumia pamoja na utaratibu wa utunzaji wa ngozi Kwa ufyonzaji wa juu, Bio‑Oil® Skincare Oil inapaswa kutumiwa kwenye ngozi iliyosafishwa. Kuchanganya Bio‑Oil® Skincare Oil na bidhaa nyingine ili ''kuifanya ifanye kazi zaidi'' kunaweza kuathiri ufanisi wake. Ikiwa unatumia kilainisha ngozi, losheni ya kukinga jua au krimu nyingine, fanya hivyo tu baada ya Bio‑Oil® Skincare Oil kufyonzwa kabisa kwenye ngozi. Kwa matumizi kwenye mwili mzima, tumia Bio‑Oil® Skincare Oil baada ya kuoga. Kutumia wakati wa ujauzito Michirizi kwenye ngozi wakati wa ujauzito inaweza kuonekana mahali popote kwenye mwili, lakini ina uwezekano mkubwa wa kuonekana kwenye fumbatio, mapaja, nyonga, mgongo wa chini, makalio na matiti. Ili kusaidia kuzuia utokeaji wa michirizi kwenye ngozi wakati wa ujauzito, inashauriwa kwamba Bio‑Oil® Skincare Oil itumike kwenye maeneo haya mara mbili kwa siku, tangu kuanza kwa miezi mitatu ya kwanza hadi baada ya kujifungua. Bio‑Oil® Skincare Oil ikitumiwa mara kwa mara itatoa pia utulivu wa ngozi inayowasha na iliyokauka, inayohusishwa na mwasho mkali wa ujauzito. Inaweza pia kutumika kwenye rangi ya ngozi isiyo sawia ambayo hutokana na kubadilika kwa homoni ambayo hutokea wakati wa ujauzito. Vitamini A na ujauzito Wanawake kwa kawaida wanapendekezewa kupunguza virutubisho vya vitamini A wakati wa ujauzito na kwa hivyo wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu kutumia bidhaa za ngozi zenye vitamini A. Dutu yoyote inayotumika kwenye ngozi ni hatari tu ikiwa iko katika viwango vya juu kuliko kiwango chake cha juu cha sumu. Kwa sababu ngozi hutoa kizuizi kikubwa cha upenyaji, sehemu ndogo tu ya vitamini A inayotumiwa ndio huingia mwilini. Kamati ya Sayansi ya Tume ya Ulaya kuhusu Usalama wa Watumiaji (SCCS) imetathmini vitamini A na michanganyiko yake, inapotumiwa kama viungo vya vipodozi. Maoni ya SCCS ni kwamba matumizi ya vitamini A katika losheni za mwili, hadi kiwango cha juu zaidi cha asilimia 0.05% ya retinoli, ni salama. Bio‑Oil® Skincare Oil ina vitamini A katika muundo wake iliyo chini ya kiwango hiki cha juu zaidi kinachoruhusiwa kwa losheni ya mwili na inaweza kutumika kwa usalama wakati wa ujauzito. Kwa kujumuisha vitamini A kwa kiwango cha chini, Bio‑Oil® Skincare Oil huwapa wanawake wajawazito faida za vitamini A bila hatari yoyote ya usalama. Mafuta ya Rosemary na ujauzito Mafuta ya Rosemary katika viwango vya juu yameonekana kuwa na uwezo wa kuongeza mtiririko wa damu, kumaanisha kuwa yana uwezo wa kuchochea hedhi na uwezekano wa kusababisha uchungu wa uzazi wa mapema. Hii ndio sababu wataalamu wa tiba mimea na mitishamba wanaotumia mafuta ya rosemary katika viwango vya juu, wanapendekeza kutoyatumia wakati wa ujauzito. Hata hivyo, kiwango cha mafuta ya rosemary katika Bio‑Oil® Skincare Oil ni cha chini sana na kwa hivyo ni salama kutumia wakati wa ujauzito. Kutumia wakati wa kunyonyesha Bio‑Oil® Skincare Oil ni salama kutumiwa kwenye mwili wakati wa kunyonyesha, lakini inapendekezwa kuepuka kutumia kwenye chuchu. Ingawa hakuna madhara yanayoweza kutokea, watoto wachanga wanaweza kuathiriwa kwa urahisi na hawapaswi kumeza Bio‑Oil® Skincare Oil, hata kwa kiasi kidogo sana. Matumizi kwa watoto wachanga na wakubwa Usalama wa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil kwa watoto chini ya umri wa miaka mitatu haujatathminiwa. Katika miaka michache ya kwanza baada ya kuzaliwa, mabadiliko mengi hufanyika katika mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kukua kwa mfumo wa kinga. Kwa hivyo inashauriwa kwamba itumiwe tu kwa watoto wenye umri wa miaka mitatu au zaidi. Bidhaa hii inapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa watoto na haipaswi kutumiwa karibu na macho au mdomo. Kutumia kwenye jua Majaribio yaliyofanywa kwenye Bio‑Oil® Skincare Oil yalionyesha kuwa bidhaa hii haiwezeshi au kuzidisha kuchomwa na jua. Kwa hivyo ni salama kutumia kukiwa na jua, hata hivyo bidhaa hii haitoi kinga dhidi ya madhara ya mionzi ya jua ya UVA na UVB na hivyo ni muhimu kutumia bidhaa hii pamoja na bidhaa nyingine za kukinga mionzi ya jua zenye sifa ya kukinga jua (SPF) ya angalau 30. Kutumia kwenye au karibu na tando telezi Bio‑Oil® Skincare Oil imeainishwa kuwa salama kwa matumizi yote, isipokuwa kwenye tando telezi. Kutumia pamoja na tibaredio au tibakemikali Ingawa Bio‑Oil® Skincare Oil haina viungo vyovyote ambavyo vinaweza kufyonza mionzi, ni vyema kwa watu wanaopata tiba ya tibaredio au tibakemikali kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia bidhaa hii. Kutumia pamoja na bidhaa za dawa Bio‑Oil® Skincare Oil ni bidhaa ya vipodozi. Kwa ushauri kuhusu kutumia bidhaa hii pamoja na kutumia bidhaa za dawa kwa wakati mmoja, ni bora kutafuta ushauri wa daktari. Kutumia kwenye ngozi inayoathirika kwa urahisi Bio‑Oil® Skincare Oil inaweza kutumika kwenye ngozi inayoathirika kwa urahisi. Katika utafiti wa mwasho wa ngozi uliofanyiwa washiriki 25 wenye umri wa miaka 18-65 walio na ngozi inayoathirika kwa urahisi, hakuna wahusika waliopata madhara yoyote mabaya kutokana na muundo huu. Kuumia kwenye ngozi yenye mafuta Bio‑Oil® Skincare Oil inaweza kutumika kwenye ngozi yenye mafuta. Katika jaribio lililofanyiwa washiriki 20 wenye umri wa miaka 18-65 wenye ngozi inayoathiriwa na chunusi, Bio‑Oil® Skincare Oil ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Kutumia kwenye ngozi inayoathiriwa na chunusi Bio‑Oil® Skincare Oil inaweza kutumika kwenye ngozi inayoathiriwa na chunusi. Katika jaribio lililofanyiwa washiriki 20 wenye umri wa miaka 18-65 wenye ngozi inayoathiriwa na chunusi, Bio‑Oil® Skincare Oil ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Katika utafiti wa makovu ya chunusi uliofanyiwa wahusika 44 wenye umri wa miaka 14–30 walio na makovu mapya ya chunusi kwenye uso; hesabu ya chunusi na matokeo ya kipimo cha mafuta ya ngozi yalionyesha kuwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil hakusababishi au kuongeza chunusi au kuongeza utoaji wa mafuta ya ngozi. Hata hivyo inashauriwa kwa watu wanaosumbuliwa na chunusi kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil.
KUTOKEA KWA MAKOVU
Kovu ni ukuaji wa kolajeni ambao hutokea kama sehemu ya kawaida ya mchakato wa kupona kufuatia jeraha kwenye ngozi. Kolajeni imeundwa kwa protini za kawaida ambazo huunda sehemu kuu ya tishu unganishi za mwili. Wakati jeraha kwenye ngozi linatokea, mwili hufanya kazi haraka iwezekanavyo kurekebisha eneo lililoathiriwa, kwa kuzingatia kuishi badala ya uponyaji kamili. Uzalishaji huo wa haraka wa kolajeni ili kukabiliana na jeraha ndio huunda makovu. Ijapokuwa kovu litapitia mabadiliko mengi kadri linavyokomaa, halitawahi kupata nguvu ya kawaida ya ngozi inayoizunguka. Vinyweleo na tezi jasho katika eneo la kovu hazitarudi tena. Kutokea kwa makovu kuna awamu nne zifuatazo: Awamu ya kuzuia damu Hii huanza mara tu baada ya jeraha kutokea na hudumu kwa saa chache, huku eneo lililojeruhiwa likijaribu kurejesha hali yake ya kawaida kwa kuzuia mishipa ya damu ili kudhibiti damu. Chembe zilizojeruhiwa wakati huo mmoja hutoa protini fulani ili kuwezesha kuganda, hivyo kuziba mishipa iliyoharibiwa na kupunguza upotezaji wa damu. Awamu ya uvimbe Wekundu na uvimbe ambao unatokea kwa kipindi cha siku tatu au nne baada ya kiwewe cha kwanza ni kiashiria kinachoonekana cha mfumo wa kinga. Chembe nyeupe za damu hutoa kemikali zinazosafisha jeraha ili kutoa uchafu na bakteria. Awamu ya kukua kwa haraka Hii huanza siku ya tatu na huendelea kwa karibu wiki tatu. Michakato mitatu tofauti hutokea kwa wakati mmoja katika awamu hii ili kufunga kidonda: Tishu unganishi: Chembe za fibroblasts (chembe zinazohusika katika kuchanganya kolajeni) huongezeka kwenye eneo la jeraha ili kuunda kolajeni kwa haraka ili kujaza jeraha. Mchakato wa kuziba: Safu ya ngozi huundwa ili kufunika jeraha. Mpunguo wa jeraha: jeraha huvutwa pamoja katika jaribio la kupunguza kasoro. Awamu ya kukomaa Awamu hii ya ''kurekebisha'' huanza baada ya takriban wiki tatu na inaweza kuendelea hadi miaka miwili kulingana na ukubwa na kina cha jeraha. Wakati huu, kolajeni huendelea kukua huku nyuzi zikipangwa upya kulingana na mikazo iliyowekwa kwenye eneo la jeraha, hivyo kuamua hali ya mwisho ya kovu. Huku kovu likifunika na kulinda eneo la jeraha, linaweza kuvurugwa kwa urahisi. Kwa ujumla tishu ya kovu huonyesha asilimia 70% ya nguvu ya mkazo wa ngozi ya kawaida.
AINA ZA MAKOVU
Kwa sababu watu hupona kitofauti, mwonekano wa mwisho wa kovu utatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mambo kama aina ya ngozi, eneo la kovu, aina ya jeraha, umri wa mtu na hata hali ya lishe itakuwa muhimu katika kuamua kovu litaonekana aje. Aina za makovu zinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo: Makovu ya kawaida Makovu haya yanaonekana yamevimba na meusi mwanzoni lakini yanalainika na kutoonekana sana baada ya muda ambayo husababisha kovu lenye mstari mwembamba. Makovu yaliyodumaa Makovu haya husababisha mibonyeo au mapengo chini ya ngozi. Mifano ni makovu yanayotokana na chunusi au tetekuwanga. Makovu yaliyoinuka Makovu haya huinuka juu ya ngozi. Sifa za makovu haya ni viwango vikubwa vya kolajeni, lakini husalia sikuzote ndani ya mipaka ya jeraha asili. Makovu mabonge Makovu mabonge yanapaswa kutofauitishwa na makovu yaliyoinuka. Ingawa pia ni makovu yaliyoinuka, sifa za makovu mabonge ni kwamba yameenea zaidi ya mipaka ya jeraha asili. Yanaweza kuendelea kukua baada ya muda na kawaida hujirudia baada ya mabonge hayo kuondolewa. Makovu ya mikazo Kovu la mikazo hutokea wakati ngozi inakaza kabisa. Mara nyingi hutokea wakati makovu yanavuka viungo, au ngozi kukunjana, kwenye pembe za kulia. Tishu ya kovu hili hukataa kunyooka na inaweza kuzuia mienendo ya kawaida. Mara nyingi makovu ya mikazo hutokea baada ya majeraha ya moto. Michirizi kwenye ngozi (Striae) Michirizi kwenye ngozi hutokea wakati wa vipindi vya mabadiliko ya haraka katika uzani (kwa mfano ukuaji wa haraka katika miaka ya ujana, ujauzito) wakati mwili unapanuka haraka kuliko ngozi inayoifunika, na kusababisha mipasuko ya ndani katika tishu za ngozi. Wakati mipasuko hii inajirekebisha yenyewe huunda makovu ambayo yanajulikana kama michirizi kwenye ngozi.
UUNDAJI WA MICHIRIZI KWENYE NGOZI
Kwa maneno ya kimatibabu michirizi kwenye ngozi, au striae, ni aina nyingine tu za makovu, hata hivyo, watu wengi huyaona kuwa tofauti na makovu. Striae ni mistari kwenye ngozi ambayo inakua katika vipindi vya upanuzi wa haraka wa ngozi, kwa mfano katika wanawake wajawazito, wajenzi wa mwili, na vijana wakati wa ukuaji wao wa haraka. Inasababishwa na kile ambacho jina like linapendekeza, kunyooka. Watu wenye ngozi nyeupe huwa na michirizi ya ngozi ya rangi ya waridi, huku watu wenye ngozi nyeusi huwa na michirizi ya ngozi ambayo ni nyeupe zaidi ya ngozi inayoizunguka. Kwa kawaida ngozi huwa nyumbufu. Unyumbufu huu hutolewa na kolajeni na elastini kwenye ngozi, ambazo ziko chini ya tishu ya ngozi. Kolajeni imeundwa na kundi la protini za kawaida na ni sehemu kuu ya tishu unganishi za mwili. Elastini, ambayo pia imeundwa kwa protini za kawaida, hupatikana pia katika tishu unganishi na hutoa sifa zake za unyumbufu. Tishu hii unganishi huwezesha ngozi kukabiliana na mwenendo endelevu wa mwili kwa kupanua na kubana, lakini wakati wa vipindi vya kuongeza uzani kwa haraka, inaweza kuwa haina muda wa kutosha wa kurekebisha, hivyo kusababisha mipasuko ya ndani katika tishu ya ngozi. Wakati mipasuko hii inajirekebisha yenyewe inaunda makovu ambayo tunayajua kama michirizi kwenye ngozi. Mfano muhimu ni ule wa springi ikinyooshwa. Ukinyoosha springi kwa kiwango fulani, kinachojulikana kama kikomo chake cha kawaida cha unyumbufu, inarudi kwenye ukubwa wake ya kawaida mara kwa mara. Hata hivyo, ikiwa utanyoosha springi zaidi ya kikomo chake cha kawaida cha unyumbufu, itakuwa imenyooshwa kabisa na haitarudi kwenye ukubwa wake wa kawaida. Ingawa michirizi kwenye mwili haiwakilishi shida kubwa ya kimatibabu, inaweza kusababisha shida ya kihisia kwa wale wanaoipata. Uwezekano wa kuipata hutofautiana kulingana na aina ya ngozi, umri, urithi, lishe na unyevu wa ngozi. Hatua za uundaji wa michirizi kwenye ngozi ni kama zifuatavyo: Hatua ya kwanza Michirizi ya mapema kwenye ngozi huonekana kuwa yenye rangi iliyofifia na pia inaweza kuwa inawasha. Ngozi iliyo karibu na michirizi hiyo pia inaweza kuonekana ''imenyooka'' na ''nyembamba''. Hatua ya pili Polepole michirizi kwenye ngozi itapanuka kwa urefu na upana na kuwa nyeusi na kuonekana zaidi. Hatua ya tatu Mara tu michirizi kwenye ngozi inapokomaa na ngozi haivutani tena, itaanza kufifia na kuwa na rangi hafifu zaidi. Inaweza pia kuonekana kuwa na mibonyeo na isiyo na umbo au urefu wa kawaida.
UUNDAJI WA MICHIRIZI KWENYE NGOZI WAKATI WA UJAUZITO
Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 50% na 90% ya wanawake wajawazito wana uwezekano wa kupata michirizi kwenye ngozi. Michirizi kwenye mwili inaweza kukua kwenye fumbatio, mapaja, nyonga, mgongo wa chini, makalio na matiti – maeneo ambayo ngozi hunyooka zaidi mwili ukibadilika wakati wa ujauzito. Ijapokuwa inaweza kuonekana mahali popote kwenye mwili, ina uwezekano mkubwa wa kuonekana katika maeneo ambayo kiasi kikubwa cha mafuta huhifadhiwa. Ijapokuwa michirizi kwenye ngozi huanza kuonekana kwa kawaida wakati wa miezi mitatu ya baadaye ya ujauzito (karibu mwezi wa sita au wa saba) baadhi ya wanawake huanza kuona michirizi kwenye ngozi ikitokea katika miezi mitatu ya kwanza. Michirizi kwenye ngozi wakati wa ujauzito pia inaweza kutokana na maandalizi ya mlango wa kizazi kwa sababu ya ongezeko la homoni. Homoni hizi huvutia maji zaidi kwenye ngozi, ambayo hutuliza mishikamano kati ya nyuzi za kolajeni. Hii inafanya iwe rahisi kwa ngozi kupasuka wakati imenyooshwa na kwa michirizi kwenye ngozi kutokea. Uwezekano wa kupata michirizi kwenye ngozi hutofautiana kulingana na aina ya ngozi, umri, urithi, lishe na unyevu wa ngozi.
UTENGENEZAJI
Utengenezaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil unafuata mahitaji ya Kanuni Bora za Utengenezaji (GMP) ya ISO 22716: 2007 kwa bidhaa za vipodozi. Malighafi zote zinazotumika katika utengenezaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil zinaambatana na Cheti cha Uchanganuzi (COA), na vifaa vyote vya ufungaji vinaambatana na Cheti cha Ukubalifu (COC). Hakuna malighafi au vifaa vya ufungaji hutolewa ili kutengenezwa hadi vipite vipimo vya kudhibiti ubora. Kila bechi ya Bio‑Oil® Skincare Oil iliyochanganywa imetengewa nambari ya kipekee ya bechi. Sampuli kutoka kwenye bechi hiyo hujaribiwa kwenye maabara ili kuangalia mwonekano, uwazi, harufu, utambulisho kwa kutumia na spectrophotometry, uzito, unato na mikrobiolojia. Sampuli huhifadhiwa kwa miaka sita. Ujazaji na ufungaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil hufanyika katika kituo kilichodhibitiwa halijoto na unyevu. Hewa hupita kupitia mfumo wa hali ya juu wa kuchuja hewa (HEPA) ili kuzuia uchafuzi wa vumbi. Wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye viwanda vya uzalishaji huvaa kofia, barakoa, ngao za uso, glavu, kanzu na vifuniko vya viatu. Sampuli huondolewa viwandani katika vipindi vya mara kwa mara na hukaguliwa na idara ya Udhibiti wa Ubora kama tahadhari dhidi ya kasoro isiyo ya kawaida. Nambari ya bechi huchapishwa kwenye chupa, katoni na shehena, na sampuli ya kubakiza kutoka kwenye kila bechi iliyotengenezwa huhifadhiwa kwa miaka sita. Hakuna uzalishaji hatari, taka hatari au maji machafu yanayotokana na uzalishaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil.
MAELEKEZO YA UHIFADHI
Bio‑Oil® Skincare Oil inapaswa kuhifadhiwa mahali baridi, mbali na miali ya moja kwa moja ya jua.
UREJELEZAJI
Bidhaa zote zinazofunga Bio‑Oil® Skincare Oil (chupa, kifuniko na katoni) zinaweza kutumiwa tena.
KIPINDI CHA BAADA YA KUFUNGUA (PAO)
Bio‑Oil® Skincare Oil ina PAO ya miezi 36. Hii ni kipindi cha muda baada ya kufungua ambacho bidhaa ni salama na inaweza kutumika bila madhara yoyote kwa mtumiaji.
UTHIBITISHO
Bio‑Oil® Skincare Oil imethibitishwa kuwa Halaal na Kosher.
MADHARA MABAYA
Ijapokuwa Bio‑Oil® Skincare Oil ina maelezo salama yanayohusu sumu na inakidhi kanuni za kimataifa kuhusu suala hili, kama ilivyo katika bidhaa zote za vipodozi, kuna hatari kwamba watumiaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil wanaweza kukumbana na madhara mabaya wakati wa kutumia bidhaa. Ikiwa madhara yoyote mabaya yatatokea, matumizi ya bidhaa yanapaswa kukomeshwa mara moja. Dalili za madhara mabaya ya ngozi zinaweza kujumuisha upele, na uvimbe, ambayo kwa kawaida hutokea katika eneo ambalo bidhaa hiyo ilitumika. Madhara haya yanaweza kuambatana na mwasho na usumbufu kidogo. Katika hali nyingi, madhara mabaya yatapungua ndani ya siku mbili hadi tatu baada ya matumizi ya bidhaa hiyo kukomeshwa. Hadi ngozi irudi hali yake ya awali, inaweza kuonekana kavu na iliyo parara madhara yakiendelea kupungua. Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu athari ya mzio inayoweza kutokea kutokana na kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil, ni busara kufanya jaribio rahisi la mzio ili kuangalia hii. Hii inafanywa kwa kutumia kiasi kidogo cha bidhaa hii kwenye kigasha cha ndani na kusubiri kwa muda wa saa 24 ili kuona ikiwa athari yoyote itatokea. Uwekundu unaoonekana wa ngozi (harara) au uvimbe mdogo wa ngozi (uvimbe) unaweza kuonyesha uwezekano wa athari ya mzio.
HAIJAJARIBIWA KWENYE WANYAMA
Bio‑Oil® Skincare Oil na malighafi zake hutengenezwa viwandani kwa kufuata kanuni za EU zinazohusiana na kuwajaribu wanyama kwa madhumuni ya vipodozi. Bio‑Oil® Skincare Oil, au viungo vyake vyovyote, havijajaribiwa kwenye wanyama na Bio‑Oil® au watoaji wao wowote wa malighafi.
HAINA BIDHAA ZA WANYAMA
Bio‑Oil® Skincare Oil haina viungo vyovyote vinavyotokana na wanyama.
KUMEZA KWA BAHATI MBAYA
Katika tukio la kumeza kwa bahati mbaya Bio‑Oil® Skincare Oil, haiwezekani kwamba athari yoyote mbaya zaidi ya hisia za kichefuchefu na kuhara zitapatikana kwa sababu Bio‑Oil® Skincare Oil haina sumu. Hata hivyo, inashauriwa kutafuta ushauri wa matibabu, hasa katika hali ya mtoto mchanga au mkubwa kumeza kwa bahati mbaya.
MABADILIKO KATIKA MWONEKANO
Bio‑Oil® Skincare Oil ina calendula, chamomile, lavender na vitu vilivyotolewa katika mimea ya rosemary na mafuta muhimu, pamoja na vitamini A, ambazo zote zinaathiriwa na mwangaza. Kuwekwa kwenye jua kunaweza kusababisha mabadiliko ya rangi baada ya muda. Hata hivyo, haina uwezekano wa kuathiri ufanisi wa bidhaa. Kama tahadhari, chupa za Bio‑Oil® Skincare Oil zina kifyonzaji cha UV. Hata hivyo bidhaa hii inapaswa kuhifadhiwa mbali na mionzi ya moja kwa moja ya jua.
TAREHE YA MWISHO KUSASISHWA
22 Agosti 2023