JINA LA NCHI

Bio‑Oil®


JINA LA BIDHAA NA UKUBWA

Skincare Oil (Natural) 25ml
Skincare Oil (Natural) 60ml
Skincare Oil (Natural) 125ml
Skincare Oil (Natural) 200ml


DALILI

Makovu Husaidia kuboresha mwonekano wa makovu mapya na ya zamani. Michirizi kwenye ngozi Husaidia kuboresha mwonekano wa michirizi kwenye ngozi. Pia husaidia kuboresha mnyumbuko wa ngozi, na hivyo kupunguza uwezekano wa michirizi kwenye ngozi kutokea. Rangi ya ngozi isiyo sawia Husaidia kuboresha mwonekano rangi ya ngozi isiyo sawia. Kuzeeka kwa ngozi Husaidia kuboresha mwonekano wa kuzeeka kwa ngozi kwenye uso na mwili. Ngozi iliyokauka Husaidia kupunguza upotezaji wa unyevu na huboresha mwonekano wa ngozi iliyokauka.


ONYESHO

Mafuta ya njano hafifu.


MUUNDO

Mchanganyiko wa mafuta ya asili.


VIUNGO

Glycine Soja Oil, Helianthus Annuus Seed Oil, Carthamus Tinctorius Seed Oil, Simmondsia Chinensis Seed Oil, Salvia Hispanica Seed Oil, Punica Granatum Seed Oil, Plukenetia Volubilis Seed Oil, Triticum Vulgare Germ Oil, Rosa Canina Fruit Oil, Calendula Officinalis Extract, Lavandula Angustifolia Oil, Rosmarinus Officinalis Leaf Oil, Anthemis Nobilis Flower Oil, Pogostemon Cablin Leaf Oil, Bisabolol, Tocopherol.


TOFAUTI YA VIUNGO VYA ASILI

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaweza kutofautiana kidogo katika rangi, harufu na uthabiti kutoka bechi moja hadi nyingine. Haya ni matokeo ya tofauti zinazotarajiwa na za kawaida katika viungo vya asili ambavyo vitatofautiana kidogo katika rangi, harufu au uthabiti kulingana na sababu kama vile msimu, hali ya udongo, mwangaza wa jua, mavuno, mifumo ya hali ya hewa, halijoto, na wakati wa mwaka.


TATHMINI YA USALAMA

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) imefanyiwa tathmini ya usalama na mtaalamu wa sumu aliyehitimu na imeainishwa kuwa salama kwa matumizi yake yaliyokusudiwa na watu wazima, ikiwa ni pamoja na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, na watoto zaidi ya umri wa miaka mitatu.


UTHIBITISHO WA UASILI

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ina uthibitisho wa ISO 16128 wa kuwa imetengenezwa kwa vitu vya asili na vitu vya asili kwa asilimia 100%.


JARIBIO LA KIMATIBABU LA MAKOVU

Kituo cha majaribio proDERM Institute for Applied Dermatological Research, Hamburg, Germany. Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa makovu. Sampuli Wahusika: Washiriki 40 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick. Umri wa makovu: yaliyotokea hivi karibuni hadi miaka 3. Maeneo ya makovu: uso au mwili kutokana na michubuko mikubwa, kukatwa au au makovu ya upasuaji. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti unaomficha mtathmini, wa kutathmini picha ya nasibu, ambao washiriki hawafichwi taarifa. Ujumuishaji wa wahusika ulifanywa na mtaalamu wa ngozi kwa kutumia Mizani ya Tathmini ya Makovu kutoka kwa mtazamo wa Mgonjwa na Daktari (POSAS). Bidhaa ilitumiwa mara mbili kila siku kwa wiki 8 kwa kusinga polepole kwa mwendo wa mviringo kwenye kovu lililochaguliwa na kwenye ngozi iliyo karibu. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika vipindi vya mara kwa mara. Lengo kuu lilikuwa kutathmini athari za bidhaa kwenye ngozi iliyochunguzwa kwa njia ya POSAS katika ziara rasmi ya kwanza na kwa wiki 2, 4 na 8. Vigezo zaidi vilivyochunguzwa mwishoni mwa utafiti vilijumuisha tathmini ya picha ya matokeo ya urembo na wakaguzi 6 wataalamu pamoja na wahusika wenyewe, na kupotoka kwa rangi ya ngozi ya makovu kwenye mazingira yao kama ilivyopimwa na Chromameter. Matokeo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural)l katika kuboresha mwonekano wa makovu. Uboreshaji muhimu kitakwimu katika POSAS (kwa kuzingatia tathmini zote za madhumuni na za kibinafsi za OSAS na PSAS) baada ya wiki 2 tu, zilizoshuhudiwa katika asilimia 94% ya wahusika. Baada ya wiki 8 asilimia 100% ya wahusika walionekana kupata nafuu, huku kiwango cha kupata nafuu kikiwa karibu mara mbili ya wiki ya 2. Unafuu endelevu na muhimu wa POSAS katika muda wa utafiti huu.


JARIBIO LA KIMATIBABU LA MICHIRIZI KWENYE NGOZI

Kituo cha majaribio proDERM Institute for Applied Dermatological Research, Hamburg, Germany. Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa michirizi kwenye ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 36 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick. Sababu za michirizi kwenye ngozi. mbalimbali (baada ya ujauzito, kuongezeka kwa uzani au ukuaji wa haraka katika miaka ya ujana). Maeneo ya michirizi kwenye ngozi: tumbo, mikono, mapaja na nyonga. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti unaomficha mtathmini, wa kutathmini picha ya nasibu, ambao washiriki hawafichwi taarifa. Ujumuishaji wa wahusika ulifanywa na daktari kulingana na Alama ya Mallol. Bidhaa ilitumiwa mara mbili kila siku kwa wiki 8 kwa kusinga polepole kwa mwendo wa mviringo kwenye striae iliyochaguliwa na kwenye ngozi iliyo karibu. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika vipindi vya mara kwa mara. Lengo kuu lilikuwa kutathmini athari za bidhaa kwenye ngozi iliyochunguzwa kwa njia ya Mizani ya Tathmini ya Makovu kutoka kwa mtazamo wa Mgonjwa na Daktari (POSAS) katika ziara rasmi ya kwanza na kwa wiki 2, 4 na 8. Kigezo zaidi kilichochunguzwa mwishoni mwa utafiti kilijumuisha tathmini ya picha ya matokeo ya urembo na wakaguzi 6 wataalamu pamoja na wahusika wenyewe. Matokeo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa michirizi kwenye ngozi. Uboreshaji muhimu kitakwimu katika POSAS (kwa kuzingatia tathmini zote za madhumuni na za kibinafsi za OSAS na PSAS) baada ya wiki 2 tu, zilizoshuhudiwa katika asilimia 71% ya wahusika. Baada ya wiki 8, asilimia 97% ya wahusika walionekana kupata nafuu, huku kiwango cha kupata nafuu kikiwa karibu mara 5 zaidi ya wiki ya 2. Unafuu endelevu na muhimu wa POSAS katika muda wa utafiti huu.


JARIBIO LA KIMATIBABU LA RANGI YA NGOZI ISIYO SAWIA

Kituo cha majaribio Thomas J. Stephens & Associates, Inc., Texas, United States of America. Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa rangi ya ngozi isiyo sawia na rangi isiyolingana wakati inatumiwa na wanawake wenye ngozi inayoathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua (kuzeeka) kwenye uso na shingo. Sampuli Wahusika: Washiriki 64 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick waliobainishwa kimatibabu kuathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua kwenye uso na shingo. Washiriki waliotibiwa kwa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) walikuwa wahusika 32 na washiriki wasiotibiwa walikuwa wahusika 32. Umri wa washiriki: 30–70. Mbinu Utafiti unaomficha mhusika, unaodhibitiwa na wa nasibu. Wahusika walishiriki katika tathmini ya kwanza ya uchunguzi ikifuatiwa na kipindi cha kuondoa matibabu cha wiki 1. Bidhaa ilitumiwa kwenye uso na shingo mara mbili kila siku kwa wiki 16. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika ziara rasmi ya kwanza. Tathmini za kimatibabu zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4 na 16. Wahusika walipewa alama za kimatibabu kwenye uso na shingo ili kuangalia rangi ya ngozi isiyo sawia na rangi isiyolingana. Picha za kidijitali pia zilichukuliwa za uso na shingo la kila mhusika, alama za picha ziltolewa baada ya kukamilika kwa utafiti. Matokeo Ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa rangi ya ngozi isiyo sawia na rangi isiyolingana katika ngozi inayoathiriwa na mwangaza jua (kuzeeka). Baada ya wiki 16 matokeo muhimu kitakwimu yalipatikana katika vigezo vyote kwenye uso na shingo, kulingana na utoaji wa alama wa kimatibabu na picha. Baada ya wiki 16, asilimia 61% ya wahusika walionyesha kupata nafuu pakubwa kitakwimu katika rangi ya ngozi isiyo sawia, na asilimia 57% katika rangi isiyolingana.


JARIBIO LA KIMATIBABU LA KUZEEKA KWA NGOZI

Kituo cha majaribio Thomas J. Stephens & Associates, Inc., Texas, United States of America. Utafiti wa 1: Uso na shingo Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ikitumiwa na wanawake wenye ngozi inayoathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua (kuzeeka) kwenye uso na shingo. Sampuli Wahusika: Washiriki 64 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick waliobainishwa kimatibabu kuathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua kwenye uso na shingo. Washiriki waliotibiwa kwa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) walikuwa wahusika 32 na washiriki wasiotibiwa walikuwa wahusika 32. Umri wa washiriki: 30–70. Mbinu Utafiti unaomficha mhusika, unaodhibitiwa na wa nasibu. Wahusika walishiriki katika tathmini ya kwanza ya uchunguzi ikifuatiwa na kipindi cha kuondoa matibabu cha wiki 1. Bidhaa ilitumiwa kwenye uso na shingo mara mbili kila siku kwa wiki 16. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika ziara rasmi ya kwanza. Tathmini za kimatibabu zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4 na 16. Wahusika walipewa alama za kimatibabu kwenye uso na shingo kwa vigezo vifuatavyo vya ufanisi: mistari laini, makunyanzi makubwa, mwonekano wa kuparara / ulaini, hisia ya kuparara / ulaini, wangavu (kutong’aa), mwonekano wa uthabiti na tathmini na mwonekano wa jumla. Picha za kidijitali pia zilichukuliwa za uso na shingo la kila mhusika, alama za picha ziltolewa baada ya kukamilika kwa utafiti. Picha zilizochukuliwa kila wakati zilipewa alama za jumla kulingana na mistari laini, makunyanzi makubwa, rangi isiyolingana, rangi ya ngozi isiyo sawia, wangavu (kutong’aa), tathmini ya jumla ya mwonekano. Matokeo Ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa jumla katika ngozi inayoathiriwa na mwangaza jua (kuzeeka) kwenye uso na shingo. Baada ya wiki 16, kikundi kilichotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare (Natural) kilishinda pakubwa kikundi kisichotibiwa katika vigezo vyote vya kimatibabu na vya kutoa alama za picha. Hii ilishuhudiwa kimatibabu kutoka wiki 4, isipokuwa kwa rangi isiyolingana. Baada ya wiki 16, asilimia 54% ya wahusika waliotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) walionyesha kuimarika pakubwa kitakwimu katika mwonekano wa jumla wa uso na shingo. Utafiti wa 2: Mwili Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil ikitumiwa kwenye ngozi ya sehemu ya juu ya kichwa, mguu wa chini na mkono na wanawake wenye ngozi inayoathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua (kuzeeka). Sampuli Wahusika: Washiriki 64 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick waliobainishwa kimatibabu kuathiriwa kidogo hadi wastani na mwanga wa jua kwenye uso na shingo. Washiriki waliotibiwa kwa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) walikuwa wahusika 32 na washiriki wasiotibiwa walikuwa wahusika 32. Umri wa washiriki: 30–70. Mbinu Utafiti unaomficha mhusika, unaodhibitiwa na wa nasibu. Wahusika walishiriki katika tathmini ya kwanza ya uchunguzi ikifuatiwa na kipindi cha kuondoa matibabu cha wiki 1. Bidhaa ilitumiwa kwenye kwa sehemu ya juu ya kichwa, miguu ya chini na mikono mara mbili kila siku kwa wiki 16. Matumizi yalifanywa chini ya usimamizi katika ziara rasmi ya kwanza. Tathmini za kimatibabu zilifanywa katika wiki ya 0, 2, 4 na 16. Wahusika walipewa alama tofauti za kimatibabu za sehemu ya juu ya kichwa, miguu ya chini na mikono kulingana na vigezo vifuatavyo vya ufanisi: mwonekano wa kuparara / ulaini, na hisia ya kuparara / ulaini, ukavu / magamba, mwonekano wa makunyanzi makubwa na tathmini ya jumla ya mwonekano. Matokeo Ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa jumla katika ngozi inayoathiriwa na mwangaza jua (kuzeeka) kwenye mwili. Baada ya wiki 2, kikundi kilichotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare (Natural) kilishinda pakubwa kikundi kisichotibiwa katika vigezo vyote vya kimatibabu na vya kutoa alama. Baada ya wiki 16, asilimia 82% ya wahusika waliotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil walionyesha kuimarika pakubwa kitakwimu katika mwonekano wa jumla wa sehemu ya juu ya kichwa, asilimia 93% katika mwonekano wa jumla wa miguu ya chini na asilimia 71% katika mwonekano wa jumla wa mikono.


JARIBIO LA KIMATIBABU LA NGOZI ILIYOKAUKA

Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Utafiti wa 1: Unyevu wa ngozi ya juu zaidi na kazi ya kuzuia Lengo Kutathmini ufanisi wa kutumia mara moja Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ili kuboresha unyevu wa ngozi ya juu zaidi (SC) na kazi ya kuzuia. Sampuli Wahusika: Washiriki 40 wa kike wenye aina mbalimbali za ngozi za Fitzpatrick. Eneo la jaribio: bidhaa inayojaribiwa ilitumiwa ndani ya mkono wa mbele wa wahusika wote. Umri wa washiriki: zaidi ya 18. Mbinu Utafiti fiche, wa nasibu, na unaodhibitiwa. Tathmini ya unyevu wa ngozi kwa kutumia Corneometer, tathmini ya kazi ya kuzia kwa kutumia Tewameter. Washiriki waliosha vigasha vyao kwa sabuni saa 2 kabla ya vipimo kuchukuliwa ili kusababisha ukavu wa ngozi. Vipimo msingi vya kifani vilichukuliwa. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilitumika kwenye eneo la ndani la mkono wa mbele wa wahusika wote. Vipimo vilichukuliwa tena mara moja baada ya matumizi ya bidhaa na saa 1 na 2 baadaye, kabla na baada ya kuondoa bidhaa. Eneo lisilotibiwa lilipimwa pia nyakati zote. Matokeo Matibabu kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) yalisababisha kuimarika pakubwa kwa ulainishaji wa ngozi na yalipunguza kwa kiasi kikubwa maji yanayotoka kwenye ngozi (TEWL), kiolezo cha kuimarika katika hali ya kizuizi cha ngozi, katika kila ukaguzi unaofuatiliwa wa majaribio, ikilinganishwa na ngozi iliyokauka. Utafiti wa 2: Mwonekano wa ngozi kavu Lengo Kutathmini ufanisi wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika kuboresha mwonekano wa ngozi iliyokauka. Sampuli Wahusika: Washiriki 25 Wazungu walioonyesha kimatibabu kuwa na ngozi kavu / kavu sana katika sehemu ya nje ya miguu ya chini. Eneo la jaribio: bidhaa inayojaribiwa ilitumiwa kwenye sehemu ya nje ya mguu wa chini ya wahusika wote. Umri wa washiriki: 25–65. Mbinu Utafiti kifani fiche, unaodhibitiwa, na wa nasibu. Tathmini za kimatibabu za ngozi iliyokauka zilifanywa na mtathmini mtaalamu wa kuangalia, tathmini ya unyevu wa ngozi na Corneometer na tathmini ya kazi ya kuzuia na Tewameter. Washiriki waliosha miguu yao kwa sabuni ili kusababisha ngozi kavu kwa kipindi cha siku 7. Vipimo msingi vya kifani vilichukuliwa. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilitumiwa mara mbili kila siku. Tathmini za kimatibabu na za kifani zilifanyika siku ya 1 na 3. Eneo lisilotibiwa lilitathminiwa pia nyakati zote. Matokeo Matibabu kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) yalisababisha kuimarika pakubwa kwa ulainishaji wa ngozi na yalipunguza kwa kiasi kikubwa TEWL, kiolezo cha kuimarika katika hali ya kizuizi cha ngozi, katika kila ukaguzi unaofuatiliwa wa majaribio, ikilinganishwa na ngozi iliyokauka. Matokeo kifani yaliyothibitishwa kwa uchanganuzi wa kimatibabu wa ukavu wa ngozi, yalitekelezwa na mtaalamu wa ngozi. Matokeo ya Utafiti wa Pamoja Kuimarika pakubwa katika mwonekano wa ngozi iliyokauka iliyotibiwa kwa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) katika utafiti wa 2 kunathibitisha ufanisi wake katika kutuliza ngozi iliyokauka. Hii inaungwa mkono zaidi na maboresho katika kazi ya kuzuia ya ngozi ya juu zaidi na TEWL katika tafiti zote mbili.


JARIBIO KWENYE NGOZI INAYOATHIRIKA KWA URAHISI

Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Kutathmini uwezo wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) kusababisha mwasho wa ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 25; 3 wa kiume na 22 wa kike, wote wakiwa na ngozi inayoathirika kwa urahisi kulingana na jaribio la kuathiriwa na asidi ya maziwa. Umri wa washiriki: 18–70. Mbinu Utafiti unaodhibitiwa. Maeneo mawili yalitathminiwa: eneo ambalo udhibiti hasi ulitumika (maji yaliyosafishwa) na eneo ambalo Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilitumika. Bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa kwenye migongo ya washiriki kwa kipindi cha saa 48 kwa kutumia Finn Chamber®. Matokeo ya ngozi yalitathminiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi, ili kutathmini mwasho wa kwanza wa ngozi kwa dakika 15, saa 1 na saa 24 baada ya kuondolewa kwa pamba. Matokeo ya ngozi yalikadiriwa kwenye mizani inayoanzia 0-4 (huku 0 ikiwa hakuna harara, uvimbe, au aina nyingine za mwasho wa ngozi, na 4 ikiwa harara na uvimbe mkali, inayoashiria mwonekano wa rangi nyekundu iliyokolea na uvimbe ulioenea zaidi ya eneo lililotumika). Matokeo Uwezo wa ngozi kustahimili Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ulichukuliwa kuwa ''usiowasha''.


JARIBIO LA KUTOSABABISHA CHUNUSI

Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Ili kujaribu ikiwa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaweza kusababisha chunusi na mabaka (chunusi). Sampuli Wahusika: Washiriki 20; 14 wa kike na 6 wa kiume wenye aina tofauti za ngozi ya Fitzpatrick na wanaoweza kuathiriwa na chunusi. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti unaodhibitiwa. Bidhaa hiyo ilitumiwa kwenye karatasi ya ufyonzaji na kupakwa kwenye eneo la juu la migongo ya washiriki. Pamba hizo ziliachwa kwa saa 48 hadi 72, zikaondolewa na kutumiwa tena. Jumla ya pamba 12 zilitumika kwa wiki 4 mfululizo. Maeneo matatu yalitathminiwa kwa kulinganisha udhibiti hasi (maji yaliyosafishwa), bidhaa inayojaribiwa (Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural)) na udhibiti chanya (kileo cha lanolini, bidhaa inayojulikana kusababisha chunusi). Matokeo ya ngozi yatathminiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi dakika 15 baada ya kuondolewa kwa kila pamba ili kulinganisha uwepo wa mabaka kabla na baada ya kutumiwa kwa kila bidhaa. Matokeo Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Eneo ambalo Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilitumika halikuonyesha tofauti kubwa ikilinganishwa na eneo la udhibiti hasi. Udhibiti chanya ulisababisha chunusi.


UTAFITI WA UFYONZAJI

Kituo cha majaribio proDERM Institute for Applied Dermatological Research, Hamburg, Germany. Lengo Kutathmini kiwango cha ufyonzaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) baada ya matumizi ya kawaida na kusugua. Sampuli Wahusika: Washiriki 100; 74 wa kike na 26 wa kiume. Eneo la jaribio: bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa ndani ya mkono wa mbele wa washiriki wote. Mbinu Utafiti fiche, wa nasibu na unaothibitiwa. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) na mafuta ya ukadiriaji yalitumiwa kwenye maeneo yaliyoteuliwa ya ndani ya mkono wa mbele wa washiriki wote. Washiriki walisugua bidhaa inayojaribiwa kwa dakika moja kila mmoja. Kisha washiriki walikadiria ufyonzaji wa bidhaa kwenye mizani ya alama 5 kuanzia ''inafyonza polepole sana'' hadi ''inafyonza haraka sana''. Matokeo Ufyonzaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) kwenye ngozi ulitathminiwa kuwa ''wa haraka sana'' au ''wa haraka'' na wengi (asilimia 64%) ya washiriki.


UTAFITI WA UWEZO WA KUZIBA

Kituo cha majaribio Rigano Laboratories, Milan, Italy. Lengo Kutathmini kama Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaonyesha kiwango sawa cha kuziba kama utando unaolinda ngozi ya kijusi. Utando unaolinda ngozi ya kijusi unazingatiwa sana na wanasayansi wa vipodozi kama ''kipimo bora zaidi'' katika ulainishaji wa ngozi kwa sababu ya kiwango chake bora cha kuziba. Mbinu Kiasi kinachojulikana cha maji kiliwekwa katika bika kikiwa kimefunikwa kwa utando unaoweza kupenyeza nusu uitwao Vitro-Skin, ambao unaiga sifa za sehemu ya juu ya ngozi ya binadamu. Kiasi sawa cha utando unaolinda ngozi ya kijusi na Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) kilitumiwa kwenye utando na kiwango cha kupoteza maji kutoka kwenye bika kilipimwa over time. Hii ililinganishwa na kiwango cha kupoteza maji bila bidhaa yoyote kwenye utando. Kiwango cha uhamishaji wa mvuke wa maji kwa kila bidhaa kilihesabiwa na kuonyeshwa katika g / m2 / h. Matokeo Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilionyesha kiwango sawa cha kuzia kama utando unaolinda ngozi ya kijusi, iliandikisha 24.9 ikilinganishwa na 27.1 ya utando unaolinda ngozi ya kijusi.


MATUMIZI

Jinsi ya kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inapaswa kusingwa kwa mwendo wa mviringo kwenye mwili hadi ifyonzwe kabisa. Inashauriwa kwamba bidhaa hiyo itumiwe mara mbili kwa siku, kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) haipaswi kutumiwa kwenye kidonda wazi au ngozi iliyokatika. Imekusudiwa kutumiwa kama kipodozi tu. Ni salama kutumia kwenye kovu mara tu ngozi iliyo juu imepona kabisa. Matokeo yatatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Muda wa kutumia Jaribio la kimatibabu la Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) limefanywa kwa kipindi cha wiki 8 na wiki 16, hivyo kuruhusu utendaji wa bidhaa hiyo kutathminiwa baada ya muda. Uchambuzi wa takwimu unaonyesha uboreshaji mkubwa katika mwonekano wa ngozi baada ya muda mfupi kama wiki mbili na kwamba uboreshaji huu unadumishwa au huongezeka kwa muda wa majaribio yote. Tumia pamoja na utaratibu wa utunzaji wa ngozi Kwa ufyonzaji wa juu, Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inapaswa kutumiwa kwenye ngozi iliyosafishwa. Kuchanganya Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) na bidhaa nyingine ili ''kuifanya ifanye kazi zaidi'' kunaweza kuathiri ufanisi wake. Ikiwa unatumia kilainisha ngozi, losheni ya kukinga jua au krimu nyingine, fanya hivyo tu baada ya Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) kufyonzwa kabisa kwenye ngozi. Kwa matumizi kwenye mwili mzima, tumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) baada ya kuoga. Kutumia wakati wa ujauzito Michirizi kwenye ngozi wakati wa ujauzito inaweza kuonekana mahali popote kwenye mwili, lakini ina uwezekano mkubwa wa kuonekana kwenye fumbatio, mapaja, nyonga, mgongo wa chini, makalio na matiti. Ili kusaidia kuzuia utokeaji wa michirizi kwenye ngozi wakati wa ujauzito, inashauriwa kwamba Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) itumike kwenye maeneo haya mara mbili kwa siku, tangu kuanza kwa miezi mitatu ya kwanza hadi baada ya kujifungua. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ikitumiwa mara kwa mara itatoa pia utulivu wa ngozi inayowasha na iliyokauka, inayohusishwa na mwasho mkali wa ujauzito. Inaweza pia kutumika kwenye rangi ya ngozi isiyo sawia ambayo hutokana na kubadilika kwa homoni ambayo hutokea wakati wa ujauzito. Vitamini A na ujauzito Wanawake kwa kawaida wanapendekezewa kupunguza virutubisho vya vitamini A wakati wa ujauzito na kwa hivyo wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu kutumia bidhaa za ngozi zenye vitamini A. Dutu yoyote inayotumika kwenye ngozi ni hatari tu ikiwa iko katika viwango vya juu kuliko kiwango chake cha juu cha sumu. Kwa sababu ngozi hutoa kizuizi kikubwa cha upenyaji, sehemu ndogo tu ya vitamini A inayotumiwa ndio huingia mwilini. Kamati ya Sayansi ya Tume ya Ulaya kuhusu Usalama wa Watumiaji (SCCS) imetathmini vitamini A na michanganyiko yake, inapotumiwa kama viungo vya vipodozi. Maoni ya SCCS ni kwamba matumizi ya vitamini A katika losheni za mwili, hadi kiwango cha juu zaidi cha asilimia 0.05% ya retinoli, ni salama. Vitamini A iliyopo katika muundo wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural), kwa sababu ya uwepo wake katika mafuta ya rosehip, iko chini ya kiwango hiki cha juu zaidi kinachoruhusiwa kwa losheni ya mwili. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaweza kutumika kwa usalama wakati wa ujauzito. Kwa kujumuisha vitamini A kwa kiwango cha chini, Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) huwapa wanawake wajawazito faida za vitamini A bila hatari yoyote ya usalama. Mafuta ya Rosemary na ujauzito Mafuta ya Rosemary katika viwango vya juu yameonekana kuwa na uwezo wa kuongeza mtiririko wa damu, kumaanisha kuwa yana uwezo wa kuchochea hedhi na uwezekano wa kusababisha uchungu wa uzazi wa mapema. Hii ndio sababu wataalamu wa tiba mimea na mitishamba wanaotumia mafuta ya rosemary katika viwango vya juu, wanapendekeza kutoyatumia wakati wa ujauzito. Hata hivyo, kiwango cha mafuta ya rosemary katika Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ni cha chini sana na kwa hivyo ni salama kutumia wakati wa ujauzito. Kutumia wakati wa kunyonyesha Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ni salama kutumiwa kwenye mwili wakati wa kunyonyesha, lakini inapendekezwa kuepuka kutumia kwenye chuchu. Ingawa hakuna madhara yanayoweza kutokea, watoto wachanga wanaweza kuathiriwa kwa urahisi na hawapaswi kumeza Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural), hata kwa kiasi kidogo sana. Matumizi kwa watoto wachanga na wakubwa Usalama wa kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) kwa watoto chini ya umri wa miaka mitatu haujatathminiwa. Katika miaka michache ya kwanza baada ya kuzaliwa, mabadiliko mengi hufanyika katika mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kukua kwa mfumo wa kinga. Kwa hivyo inashauriwa kwamba itumiwe tu kwa watoto wenye umri wa miaka mitatu au zaidi. Bidhaa hii inapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa watoto na haipaswi kutumiwa karibu na macho au mdomo. Kutumia kwenye jua Majaribio yaliyofanywa kwenye Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) yalionyesha kuwa bidhaa hii haiwezeshi au kuzidisha kuchomwa na jua. Kwa hivyo ni salama kutumia kukiwa na jua, hata hivyo bidhaa hii haitoi kinga dhidi ya madhara ya mionzi ya jua ya UVA na UVB na hivyo ni muhimu kutumia bidhaa hii pamoja na bidhaa nyingine za kukinga mionzi ya jua zenye sifa ya kukinga jua (SPF) ya angalau 30. Kutumia kwenye au karibu na tando telezi Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) imeainishwa kuwa salama kwa matumizi yote, isipokuwa kwenye tando telezi. Kutumia pamoja na tibaredio au tibakemikali Ingawa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) haina viungo vyovyote ambavyo vinaweza kufyonza mionzi, ni vyema kwa watu wanaopata tiba ya tibaredio au tibakemikali kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia bidhaa hii. Kutumia pamoja na bidhaa za dawa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ni bidhaa ya vipodozi. Kwa ushauri kuhusu kutumia bidhaa hii pamoja na kutumia bidhaa za dawa kwa wakati mmoja, ni bora kutafuta ushauri wa daktari. Kutumia kwenye ngozi inayoathirika kwa urahisi Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaweza kutumika kwenye ngozi inayoathirika kwa urahisi. Katika utafiti wa mwasho wa ngozi uliofanyiwa washiriki 25 wenye umri wa miaka 18-70 walio na ngozi inayoathirika kwa urahisi, hakuna wahusika waliopata madhara yoyote mabaya kutokana na muundo huu. Kuumia kwenye ngozi yenye mafuta Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaweza kutumika kwenye ngozi yenye mafuta. Katika jaribio lililofanyiwa washiriki 20 wenye umri wa miaka 18-65 wenye ngozi inayoathiriwa na chunusi, Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Kutumia kwenye ngozi inayoathiriwa na chunusi Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inaweza kutumika kwenye ngozi inayoathiriwa na chunusi. Katika jaribio lililofanyiwa washiriki 20 wenye umri wa miaka 18-65 wenye ngozi inayoathiriwa na chunusi, Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilipatikana kuwa haisababishi chunusi.


KUTOKEA KWA MAKOVU

Kovu ni ukuaji wa kolajeni ambao hutokea kama sehemu ya kawaida ya mchakato wa kupona kufuatia jeraha kwenye ngozi. Kolajeni imeundwa kwa protini za kawaida ambazo huunda sehemu kuu ya tishu unganishi za mwili. Wakati jeraha kwenye ngozi linatokea, mwili hufanya kazi haraka iwezekanavyo kurekebisha eneo lililoathiriwa, kwa kuzingatia kuishi badala ya uponyaji kamili. Uzalishaji huo wa haraka wa kolajeni ili kukabiliana na jeraha ndio huunda makovu. Ijapokuwa kovu litapitia mabadiliko mengi kadri linavyokomaa, halitawahi kupata nguvu ya kawaida ya ngozi inayoizunguka. Vinyweleo na tezi jasho katika eneo la kovu hazitarudi tena. Kutokea kwa makovu kuna awamu nne zifuatazo: Awamu ya kuzuia damu Hii huanza mara tu baada ya jeraha kutokea na hudumu kwa saa chache, huku eneo lililojeruhiwa likijaribu kurejesha hali yake ya kawaida kwa kuzuia mishipa ya damu ili kudhibiti damu. Chembe zilizojeruhiwa wakati huo mmoja hutoa protini fulani ili kuwezesha kuganda, hivyo kuziba mishipa iliyoharibiwa na kupunguza upotezaji wa damu. Awamu ya uvimbe Wekundu na uvimbe ambao unatokea kwa kipindi cha siku tatu au nne baada ya kiwewe cha kwanza ni kiashiria kinachoonekana cha mfumo wa kinga. Chembe nyeupe za damu hutoa kemikali zinazosafisha jeraha ili kutoa uchafu na bakteria. Awamu ya kukua kwa haraka Hii huanza siku ya tatu na huendelea kwa karibu wiki tatu. Michakato mitatu tofauti hutokea kwa wakati mmoja katika awamu hii ili kufunga kidonda: Tishu unganishi: Chembe za fibroblasts (chembe zinazohusika katika kuchanganya kolajeni) huongezeka kwenye eneo la jeraha ili kuunda kolajeni kwa haraka ili kujaza jeraha. Mchakato wa kuziba: Safu ya ngozi huundwa ili kufunika jeraha. Mpunguo wa jeraha: jeraha huvutwa pamoja katika jaribio la kupunguza kasoro. Awamu ya kukomaa Awamu hii ya ''kurekebisha'' huanza baada ya takriban wiki tatu na inaweza kuendelea hadi miaka miwili kulingana na ukubwa na kina cha jeraha. Wakati huu, kolajeni huendelea kukua huku nyuzi zikipangwa upya kulingana na mikazo iliyowekwa kwenye eneo la jeraha, hivyo kuamua hali ya mwisho ya kovu. Huku kovu likifunika na kulinda eneo la jeraha, linaweza kuvurugwa kwa urahisi. Kwa ujumla tishu ya kovu huonyesha asilimia 70% ya nguvu ya mkazo wa ngozi ya kawaida.


AINA ZA MAKOVU

Kwa sababu watu hupona kitofauti, mwonekano wa mwisho wa kovu utatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mambo kama aina ya ngozi, eneo la kovu, aina ya jeraha, umri wa mtu na hata hali ya lishe itakuwa muhimu katika kuamua kovu litaonekana aje. Aina za makovu zinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo: Makovu ya kawaida Makovu haya yanaonekana yamevimba na meusi mwanzoni lakini yanalainika na kutoonekana sana baada ya muda ambayo husababisha kovu lenye mstari mwembamba. Makovu yaliyodumaa Makovu haya husababisha mibonyeo au mapengo chini ya ngozi. Mifano ni makovu yanayotokana na chunusi au tetekuwanga. Makovu yaliyoinuka Makovu haya huinuka juu ya ngozi. Sifa za makovu haya ni viwango vikubwa vya kolajeni, lakini husalia sikuzote ndani ya mipaka ya jeraha asili. Makovu mabonge Makovu mabonge yanapaswa kutofauitishwa na makovu yaliyoinuka. Ingawa pia ni makovu yaliyoinuka, sifa za makovu mabonge ni kwamba yameenea zaidi ya mipaka ya jeraha asili. Yanaweza kuendelea kukua baada ya muda na kawaida hujirudia baada ya mabonge hayo kuondolewa. Makovu ya mikazo Kovu la mikazo hutokea wakati ngozi inakaza kabisa. Mara nyingi hutokea wakati makovu yanavuka viungo, au ngozi kukunjana, kwenye pembe za kulia. Tishu ya kovu hili hukataa kunyooka na inaweza kuzuia mienendo ya kawaida. Mara nyingi makovu ya mikazo hutokea baada ya majeraha ya moto. Michirizi kwenye ngozi (Striae) Michirizi kwenye ngozi hutokea wakati wa vipindi vya mabadiliko ya haraka katika uzani (kwa mfano ukuaji wa haraka katika miaka ya ujana, ujauzito) wakati mwili unapanuka haraka kuliko ngozi inayoifunika, na kusababisha mipasuko ya ndani katika tishu za ngozi. Wakati mipasuko hii inajirekebisha yenyewe huunda makovu ambayo yanajulikana kama michirizi kwenye ngozi.


UUNDAJI WA MICHIRIZI KWENYE NGOZI

Kwa maneno ya kimatibabu michirizi kwenye ngozi, au striae, ni aina nyingine tu za makovu, hata hivyo, watu wengi huyaona kuwa tofauti na makovu. Striae ni mistari kwenye ngozi ambayo inakua katika vipindi vya upanuzi wa haraka wa ngozi, kwa mfano katika wanawake wajawazito, wajenzi wa mwili, na vijana wakati wa ukuaji wao wa haraka. Inasababishwa na kile ambacho jina like linapendekeza, kunyooka. Watu wenye ngozi nyeupe huwa na michirizi ya ngozi ya rangi ya waridi, huku watu wenye ngozi nyeusi huwa na michirizi ya ngozi ambayo ni nyeupe zaidi ya ngozi inayoizunguka. Kwa kawaida ngozi huwa nyumbufu. Unyumbufu huu hutolewa na kolajeni na elastini kwenye ngozi, ambazo ziko chini ya tishu ya ngozi. Kolajeni imeundwa na kundi la protini za kawaida na ni sehemu kuu ya tishu unganishi za mwili. Elastini, ambayo pia imeundwa kwa protini za kawaida, hupatikana pia katika tishu unganishi na hutoa sifa zake za unyumbufu. Tishu hii unganishi huwezesha ngozi kukabiliana na mwenendo endelevu wa mwili kwa kupanua na kubana, lakini wakati wa vipindi vya kuongeza uzani kwa haraka, inaweza kuwa haina muda wa kutosha wa kurekebisha, hivyo kusababisha mipasuko ya ndani katika tishu ya ngozi. Wakati mipasuko hii inajirekebisha yenyewe inaunda makovu ambayo tunayajua kama michirizi kwenye ngozi. Mfano muhimu ni ule wa springi ikinyooshwa. Ukinyoosha springi kwa kiwango fulani, kinachojulikana kama kikomo chake cha kawaida cha unyumbufu, inarudi kwenye ukubwa wake ya kawaida mara kwa mara. Hata hivyo, ikiwa utanyoosha springi zaidi ya kikomo chake cha kawaida cha unyumbufu, itakuwa imenyooshwa kabisa na haitarudi kwenye ukubwa wake wa kawaida. Ingawa michirizi kwenye mwili haiwakilishi shida kubwa ya kimatibabu, inaweza kusababisha shida ya kihisia kwa wale wanaoipata. Uwezekano wa kuipata hutofautiana kulingana na aina ya ngozi, umri, urithi, lishe na unyevu wa ngozi. Hatua za uundaji wa michirizi kwenye ngozi ni kama zifuatavyo: Hatua ya kwanza Michirizi ya mapema kwenye ngozi huonekana kuwa yenye rangi iliyofifia na pia inaweza kuwa inawasha. Ngozi iliyo karibu na michirizi hiyo pia inaweza kuonekana ''imenyooka'' na ''nyembamba''. Hatua ya pili Polepole michirizi kwenye ngozi itapanuka kwa urefu na upana na kuwa nyeusi na kuonekana zaidi. Hatua ya tatu Mara tu michirizi kwenye ngozi inapokomaa na ngozi haivutani tena, itaanza kufifia na kuwa na rangi hafifu zaidi. Inaweza pia kuonekana kuwa na mibonyeo na isiyo na umbo au urefu wa kawaida.


UUNDAJI WA MICHIRIZI KWENYE NGOZI WAKATI WA UJAUZITO

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 50% na 90% ya wanawake wajawazito wana uwezekano wa kupata michirizi kwenye ngozi. Michirizi kwenye mwili inaweza kukua kwenye fumbatio, mapaja, nyonga, mgongo wa chini, makalio na matiti – maeneo ambayo ngozi hunyooka zaidi mwili ukibadilika wakati wa ujauzito. Ijapokuwa inaweza kuonekana mahali popote kwenye mwili, ina uwezekano mkubwa wa kuonekana katika maeneo ambayo kiasi kikubwa cha mafuta huhifadhiwa. Ijapokuwa michirizi kwenye ngozi huanza kuonekana kwa kawaida wakati wa miezi mitatu ya baadaye ya ujauzito (karibu mwezi wa sita au wa saba) baadhi ya wanawake huanza kuona michirizi kwenye ngozi ikitokea katika miezi mitatu ya kwanza. Michirizi kwenye ngozi wakati wa ujauzito pia inaweza kutokana na maandalizi ya mlango wa kizazi kwa sababu ya ongezeko la homoni. Homoni hizi huvutia maji zaidi kwenye ngozi, ambayo hutuliza mishikamano kati ya nyuzi za kolajeni. Hii inafanya iwe rahisi kwa ngozi kupasuka wakati imenyooshwa na kwa michirizi kwenye ngozi kutokea. Uwezekano wa kupata michirizi kwenye ngozi hutofautiana kulingana na aina ya ngozi, umri, urithi, lishe na unyevu wa ngozi.


UTENGENEZAJI

Utengenezaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) unafuata mahitaji ya Kanuni Bora za Utengenezaji (GMP) ya ISO 22716: 2007 kwa bidhaa za vipodozi. Malighafi zote zinazotumika katika utengenezaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) zinaambatana na Cheti cha Uchanganuzi (COA), na vifaa vyote vya ufungaji vinaambatana na Cheti cha Ukubalifu (COC). Hakuna malighafi au vifaa vya ufungaji hutolewa ili kutengenezwa hadi vipite vipimo vya kudhibiti ubora. Kila bechi ya Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) iliyochanganywa imetengewa nambari ya kipekee ya bechi. Sampuli kutoka kwenye bechi hiyo hujaribiwa kwenye maabara ili kuangalia mwonekano, uwazi, harufu, utambulisho kwa kutumia na spectrophotometry, uzito, unato na mikrobiolojia. Sampuli huhifadhiwa kwa miaka minne. Ujazaji na ufungaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) hufanyika katika kituo kilichodhibitiwa halijoto na unyevu. Hewa hupita kupitia mfumo wa hali ya juu wa kuchuja hewa (HEPA) ili kuzuia uchafuzi wa vumbi. Wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye viwanda vya uzalishaji huvaa kofia, barakoa, ngao za uso, glavu, kanzu na vifuniko vya viatu. Sampuli huondolewa viwandani katika vipindi vya mara kwa mara na hukaguliwa na idara ya Udhibiti wa Ubora kama tahadhari dhidi ya kasoro isiyo ya kawaida. Nambari ya bechi huchapishwa kwenye chupa, katoni na shehena, na sampuli ya kubakiza kutoka kwenye kila bechi iliyotengenezwa huhifadhiwa kwa miaka minne. Hakuna uzalishaji hatari, taka hatari au maji machafu yanayotokana na uzalishaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural).


MAELEKEZO YA UHIFADHI

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) inapaswa kuhifadhiwa mahali baridi, mbali na miali ya moja kwa moja ya jua.


UREJELEZAJI

Bidhaa zote zinazofunga Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) (chupa, kifuniko na katoni) zinaweza kutumiwa tena.


KIPINDI CHA BAADA YA KUFUNGUA (PAO)

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ina PAO ya miezi 12. Hii ni kipindi cha muda baada ya kufungua ambacho bidhaa ni salama na inaweza kutumika bila madhara yoyote kwa mtumiaji.


UTHIBITISHO

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) imethibitishwa kuwa Halaal na Kosher.


MADHARA MABAYA

Ijapokuwa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ina maelezo salama yanayohusu sumu na inakidhi kanuni za kimataifa kuhusu suala hili, kama ilivyo katika bidhaa zote za vipodozi, kuna hatari kwamba watumiaji wa Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) wanaweza kukumbana na madhara mabaya wakati wa kutumia bidhaa. Ikiwa madhara yoyote mabaya yatatokea, matumizi ya bidhaa yanapaswa kukomeshwa mara moja. Dalili za madhara mabaya ya ngozi zinaweza kujumuisha upele, na uvimbe, ambayo kwa kawaida hutokea katika eneo ambalo bidhaa hiyo ilitumika. Madhara haya yanaweza kuambatana na mwasho na usumbufu kidogo. Katika hali nyingi, madhara mabaya yatapungua ndani ya siku mbili hadi tatu baada ya matumizi ya bidhaa hiyo kukomeshwa. Hadi ngozi irudi hali yake ya awali, inaweza kuonekana kavu na iliyo parara madhara yakiendelea kupungua. Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu athari ya mzio inayoweza kutokea kutokana na kutumia Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural), ni busara kufanya jaribio rahisi la mzio ili kuangalia hii. Hii inafanywa kwa kutumia kiasi kidogo cha bidhaa hii kwenye kigasha cha ndani na kusubiri kwa muda wa saa 24 ili kuona ikiwa athari yoyote itatokea. Uwekundu unaoonekana wa ngozi (harara) au uvimbe mdogo wa ngozi (uvimbe) unaweza kuonyesha uwezekano wa athari ya mzio.


HAIJAJARIBIWA KWENYE WANYAMA

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) na malighafi zake hutengenezwa viwandani kwa kufuata kanuni za EU zinazohusiana na kuwajaribu wanyama kwa madhumuni ya vipodozi. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural), au viungo vyake vyovyote, havijajaribiwa kwenye wanyama na Bio‑Oil® au watoaji wao wowote wa malighafi.


HAINA BIDHAA ZA WANYAMA

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) haina viungo vyovyote vinavyotokana na wanyama.


KUMEZA KWA BAHATI MBAYA

Katika tukio la kumeza kwa bahati mbaya Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural), haiwezekani kwamba athari yoyote mbaya zaidi ya hisia za kichefuchefu na kuhara zitapatikana kwa sababu Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) haina sumu. Hata hivyo, inashauriwa kutafuta ushauri wa matibabu, hasa katika hali ya mtoto mchanga au mkubwa kumeza kwa bahati mbaya.


MABADILIKO KATIKA MWONEKANO

Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ina calendula, chamomile, lavender, patchouli na vitu vilivyotolewa katika mimea ya rosemary na mafuta muhimu, na hata pia vitamini A kwa njia ya mafuta ya rosehip, ambazo zote zinaathiriwa na mwangaza. Kuwekwa kwenye jua kunaweza kusababisha mabadiliko ya rangi baada ya muda. Hata hivyo, haina uwezekano wa kuathiri ufanisi wa bidhaa. Kama tahadhari, chupa za Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) zina kifyonzaji cha UV. Hata hivyo bidhaa hii inapaswa kuhifadhiwa mbali na mionzi ya moja kwa moja ya jua.


TAREHE YA MWISHO KUSASISHWA

22 Agosti 2023